Wednesday, November 28, 2012

Thursday, August 2, 2012



Karibu sana ndugu wateja kampuni ya Asak Enterprises Co.Ltd iliyoko Maeneo ya Mikocheni karibu na kwa Mwl Nyerere ASAK company ni mabingwa wa matairi mapya ya magari pamoja na huduma zao za kisasa karibuni sana.


Thursday, June 14, 2012

                                                     Area where are Helicopter Crash

Kenya minister George Saitoti killed in air Crash


Tuesday, May 1, 2012

Aliyekua Mbunge wa Sumbawanga Mjini(CCM)Aeshi Hillary
Aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM) Aeshi Hillary  amevuliwa ubunge na mahakama, kufuati hukumu ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Sumbawanga Mjini dhidi ya Mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye alidai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.

    Miongoni mwa madai mengine ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki.

Vijana wakionyesha bango la kuwataka 'magamba' waendelee kujitoa CCM..
 Wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa Rais kuwajibika inapobidi.
 Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.
 Nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea  Vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika jana kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.

...mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Pah One
.....licha ya kimvua, burudani ziliendelea kama kawa...Michael Jackson wa Bongo akifanya vitu vyake
.....msanii Tumbulo akiingia kistaili jukwaani
 Mwanamuziki Diamond Akishukuru baada ya kutua ukumbi wa Dar Live
 Hapa akionyesha ishara ya kuwasalimia mashabiki wake kwa heshima.
 Mwanamuziki Diamond akiwa kwenye helikopta tayari kuelekea Dar Live.
Mwanamuziki Diamond akiingia ndani ya ukumbi wa DARLIVE muda mfupi baada ya kutua kweanye helikopta
Mwanamuziki Diamond  anayevuma kwa sasa hapa nchini  kifanya onyesho zito na la kukata na shoka mbele ya mashabiki wake  kwenye ukumbi wa Dar Live, onyesho hilo  lililofanyika jana siku ya jumapili na kuvuta hisia za mashabiki wake lukuki waliojitokeza kumshuhudia akishuka na helikopta kama ilivyokuwa imetangazwa na waandaji wa onyesho hilo.
...ilikuwa ni shoo iliyopandisha mzuka wa mashabiki kupita kawaida
Katika shoo zote za Dar Live, Diamond amevunja rekodi ya idadi ya mashabiki
 Wacheza shoo wake wakifanya vitu vyao jukwaani.
....Timbulo akiwa juu ya jukwaa..
...licha ya mvua kunyesha wakati fulani, mashabiki hawakukubali kuondoka bila kumuona Diamond!
Timbulo akifanya vitu na dancers wake
...hii ndivyo ilivyokuwa Dar Live usiku wa kuamkia leo.Picha na Habari na Richard Bukos, Issa Mnally

 Mbunge Tundu Lissu akihutubia mkutano viwanja vya stendi ya zamani mjini Singida, tangu mahakama kuu impe ushindi dhidi y
 Mbunge wa Singida mashariki(CHADEMA) Tundu Lissu(wa pili kulia),akiingia kwenye viwanja wa stendi ya zamani mjini Singida kwa ajili ya mkutano
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack
Na Elisante John Aprili 30,2012.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa wito kwa viongozi na wanachama ‘safi’, walio ndani ya CCM, wajiunge mapema na CHADEMA ili waikomboe nchi, kutoka kwa wezi na mafisadi wa fedha za umma.
Mnadhimu mkuu, kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitoa rai hiyo kwenye mkutano wa hadhara, aliufanya eneo la stendi ya zamani, mjini Singida, kwa lengo la kukiimarisha chama, bada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi.
Lissu ambaye pia ni mbunge Singida mashariki, aliwashauri  wajiondoe mapema, badala ya kung’ang’ania huko, kusubiri CHADEMA itawale nchi, halafu ndio wajitokeze kusema na wao ni wafuasi wa chama hicho.
Pia aliwaomba viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA hivi sasa wachukue tahadhari, vinginevyo watapata madhara makubwa, ikiwemo hata kupoteza maisha yao.
Alisema kitendo cha kuuawa kwa mwenyekiti wao huko Usa river, mkoani Arusha na kukatwa katwa kwa panga wabunge wa CHADEMA mkoani Mwanza, ni onyo kwa wanachama na viongozi wa chama hicho.
“Vita hii ni kubwa, lazima tuielewe, kuanzia sasa kaeni chonjo, vinginevyo CHADEMA tutauawa, mwenyekiti wetu kule Arusha amechinjwa na wabunge wetu huko Mwanza wamekatwa katwa mapanga, tena mbele ya polisi….tuangalie sana,”alitahadharisha Lissu.
Kuhusu ushindi wa kesi iliyomkabili, ambayo ni moja ya mashauri 14 yaliyofunguliwa, kati ya majimbo 23 ya CHADEMA nchini, Lissu aliishukuru mahakama kumuona hana hatia, ingawa anaamini wadai wamepoteza fedha nyingi, zinazofikia zaidi ya Sh. Milioni 200, ili ubunge wake utenguliwe.
Huo ulikuwa mkutano wa kwanza kufanyika Singida mjini na watatu kimkoa, tangu mahakama kuu, kanda ya Dodoma, kupitia Jaji Moses Mzuna wa Moshi, Mkoani Kilimanjaro, kufutilia mbali shauri la kupinga ubunge, alilofunguliwa na wanachama wawili wa CCM.
Na Elisante John.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongoza kikao  cha Investment Forum SAGCOT Local Investors, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Aprili 30, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Rais Jakaya Kikwete akimnadi aliyekua mbunge wa sumbawanga Mjini Aeshy Hilaly(CCM) Kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu Mwaka Jana.
Hukumu ya kupinga matokeo ya ubunge wa sumbawanga mjini wa Aeshy Hilaly Halphany CCM dhidi ya mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye anadai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.

Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo, mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika. Mahakama imemvua ubunge mbunge wa CCM Bw. Aheshy Hilaly.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Hani Abdalla Mohammed  Mu'minah,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Nchini Tanzania Mohsen Movahhed Ghomi.aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo na  Rais.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Hani Abdalla Mohammed  Mu'minah,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar jana kujitambulisha kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Nchini Tanzania Mohsen Movahhed Ghomi.aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar jana kwa mazungumzo na  Rais.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar.