Aliyekua Mbunge wa Sumbawanga Mjini(CCM)Aeshi Hillary
Aliyekuwa
Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM) Aeshi Hillary amevuliwa
ubunge na mahakama, kufuati hukumu ya kupinga matokeo ya Ubunge wa
Sumbawanga Mjini dhidi ya Mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema
ambaye alidai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.
Miongoni mwa madai mengine ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi
mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa
ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki,
vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki.
Vijana wakionyesha bango la kuwataka 'magamba' waendelee kujitoa CCM..
Wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa Rais kuwajibika inapobidi.
Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.
Nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya
CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea Vijana wa Shirikisho la
CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika jana
kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia
ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa
kuhusika na upotefu wa fedha za umma.
...mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Pah One
.....licha ya kimvua, burudani ziliendelea kama kawa...Michael Jackson wa Bongo akifanya vitu vyake
.....msanii Tumbulo akiingia kistaili jukwaani
Mwanamuziki Diamond Akishukuru baada ya kutua ukumbi wa Dar Live
Hapa akionyesha ishara ya kuwasalimia mashabiki wake kwa heshima.
Mwanamuziki Diamond akiwa kwenye helikopta tayari kuelekea Dar Live.
Mwanamuziki Diamond akiingia ndani ya ukumbi wa DARLIVE muda mfupi baada ya kutua kweanye helikopta
Mwanamuziki Diamond anayevuma kwa sasa hapa nchini kifanya onyesho
zito na la kukata na shoka mbele ya mashabiki wake kwenye ukumbi wa
Dar Live, onyesho hilo lililofanyika jana siku ya jumapili na kuvuta
hisia za mashabiki wake lukuki waliojitokeza kumshuhudia akishuka na
helikopta kama ilivyokuwa imetangazwa na waandaji wa onyesho hilo.
...ilikuwa ni shoo iliyopandisha mzuka wa mashabiki kupita kawaida
Katika shoo zote za Dar Live, Diamond amevunja rekodi ya idadi ya mashabiki
Wacheza shoo wake wakifanya vitu vyao jukwaani.
....Timbulo akiwa juu ya jukwaa..
...licha ya mvua kunyesha wakati fulani, mashabiki hawakukubali kuondoka bila kumuona Diamond!
Timbulo akifanya vitu na dancers wake
...hii ndivyo ilivyokuwa Dar Live usiku wa kuamkia leo.Picha na Habari na Richard Bukos, Issa Mnally
Mbunge Tundu Lissu akihutubia mkutano viwanja vya stendi ya zamani mjini Singida, tangu mahakama kuu impe ushindi dhidi y
Mbunge
wa Singida mashariki(CHADEMA) Tundu Lissu(wa pili kulia),akiingia kwenye viwanja
wa stendi ya zamani mjini Singida kwa ajili ya mkutano
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack
Na Elisante John Aprili 30,2012.
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa wito kwa viongozi na
wanachama ‘safi’, walio ndani ya CCM, wajiunge mapema na CHADEMA ili
waikomboe nchi, kutoka kwa wezi na mafisadi wa fedha za umma.
Mnadhimu
mkuu, kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitoa rai hiyo kwenye
mkutano wa hadhara, aliufanya eneo la stendi ya zamani, mjini Singida,
kwa lengo la kukiimarisha chama, bada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi.
Lissu
ambaye pia ni mbunge Singida mashariki, aliwashauri wajiondoe mapema,
badala ya kung’ang’ania huko, kusubiri CHADEMA itawale nchi, halafu
ndio wajitokeze kusema na wao ni wafuasi wa chama hicho.
Pia aliwaomba
viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA hivi sasa wachukue
tahadhari, vinginevyo watapata madhara makubwa, ikiwemo hata kupoteza
maisha yao.
Alisema
kitendo cha kuuawa kwa mwenyekiti wao huko Usa river, mkoani Arusha na
kukatwa katwa kwa panga wabunge wa CHADEMA mkoani Mwanza, ni onyo kwa
wanachama na viongozi wa chama hicho.
“Vita
hii ni kubwa, lazima tuielewe, kuanzia sasa kaeni chonjo, vinginevyo
CHADEMA tutauawa, mwenyekiti wetu kule Arusha amechinjwa na wabunge wetu
huko Mwanza wamekatwa katwa mapanga, tena mbele ya polisi….tuangalie
sana,”alitahadharisha Lissu.
Kuhusu
ushindi wa kesi iliyomkabili, ambayo ni moja ya mashauri 14
yaliyofunguliwa, kati ya majimbo 23 ya CHADEMA nchini, Lissu aliishukuru
mahakama kumuona hana hatia, ingawa anaamini wadai wamepoteza fedha
nyingi, zinazofikia zaidi ya Sh. Milioni 200, ili ubunge wake
utenguliwe.
Huo
ulikuwa mkutano wa kwanza kufanyika Singida mjini na watatu kimkoa,
tangu mahakama kuu, kanda ya Dodoma, kupitia Jaji Moses Mzuna wa Moshi,
Mkoani Kilimanjaro, kufutilia mbali shauri la kupinga ubunge,
alilofunguliwa na wanachama wawili wa CCM.
Na Elisante John.
Rais Jakaya Kikwete akimnadi aliyekua mbunge wa sumbawanga Mjini Aeshy Hilaly(CCM) Kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu Mwaka Jana.
Hukumu
ya kupinga matokeo ya ubunge wa sumbawanga mjini wa Aeshy Hilaly
Halphany CCM dhidi ya mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye
anadai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.
Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo, mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.
Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo, mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika. Mahakama imemvua ubunge mbunge wa CCM Bw. Aheshy Hilaly.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa
Saudi Arabia Nchini Tanzania Hani Abdalla Mohammed Mu'minah,aliyefika
Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Nchini Tanzania Mohsen Movahhed
Ghomi.aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo na Rais.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Hani Abdalla Mohammed
Mu'minah,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar jana kujitambulisha kwa
Rais.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Nchini
Tanzania Mohsen Movahhed Ghomi.aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar jana kwa
mazungumzo na Rais.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar.
No comments:
Post a Comment